11. Mazingatio yanayopatikana katika kisa cha swahabah aliyemjamii mkewe mchana wa Ramadhaan

Katika kisa hiki kuna mazingatio ikiwa ni pamoja na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwa mkali kwa mtu huyu, hakumkemea na wala hakumkaripia. Kwa kuwa amekuja hali ya kuwa ni mwenye kutubia na ni mwenye kujuta. Kuna tofauti kati ya mtu mkaidi na ambaye yuko katika hali ya salama aliyekuja akitaka tumsaidie na akituomba tumuokoe na yale aliyotumbukia ndani yake. Ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitangamana naye namna hii ambapo alirudi kwa familia yake akiwa na zawadi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo ni tende hizi zilizokuwa ni faradhi kwake. Ingelikuwa sio kwa sababu ya umasikini wake basi ingelikuwa ni juu yake kuwalisha masikini sitini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Dawr-ul-Mar´ah fiy Iswlaah-il-Mujtama´ https://www.sahab.net/home/?p=806
  • Imechapishwa: 02/02/2017