11. Mara Smith akanyamaza na kutoonekana

Smith akasema: “Injili inathibitisha kuwa ´Iysaa ni mwana wa Allaah na ni mmoja katika utatu.” Nikamwambia: “Mimi sikusoma Injili, lakini nina yakini kabisa ya kwamba Injili ni kweli, inatoka kwa Allaah na hivyo ni lazima iafikiane na Qur-aan juu ya umoja wa Allaah na uanadamu wa ´Iysaa bin Maryam. Akanambia: “Hivi ndivyo mlivyo waislamu. Ushabiki wenu unakuzuieni kusoma Taurati na Injili. Kuhusu mimi nina Qur-aan kwa lugha tatu tofauti.” Nikamwambia: “Injili kwa kiarabu ni dhaifu na haieleweki. Kuhusu Injili kwa kingereza hivi mimi najifunza kingereza ili niweze kuisoma.” Akanambia: “Niahidi kuisoma. Mimi nitakuagizia nakala kutoka London. Itafika baada ya mwezi mmoja.”

Nikamuahidi. Pindi nakala ilipofika akanitumia nayo pamoja na barua iliokuwa ndani ilikuwa imeandikwa kwa kingereza:

“Ninamuomba Allaah akupe baraka nyingi kwa kitabu hiki.”

Nikaanza kuisoma. Neno nililokuwa sifahamu nilikuwa nikiliangalia kwenye kamusi kisha nikilisoma kwa mara ya tatu. Nimeyataja mambo hayo kwenye kijitabu kinachoitwa “Hawaash Shattaa ´alaa Injiyl Mataa”[1] na nikaieneza kwenye gazeti ” ash-Shubbhaan al-Muslimuun” iliyochapishwa na rafiki yetu Twaahaa al-Fayyaadhw huko al-Basrah. Pindi nilipomweleza Shakiyb Arslaan[2] (Rahimahu Allaah) kuhusu taaliki hizi akaniuliza nazo. Nikamweleza kuwa zilinipotea kwenye duka la kuchapisha na akawa amesikitika sana juu ya hilo. Mimi sasa niko tayari kuandika taaliki mfano wa ile au hata bora kuliko ile lakini wengi katika ndugu zetu waislamu hawajali kuitetea dini yao wala kumsaidia yule mwenye kuitetea; bali hata wanamkosesha nusura.

Nilipopata kitabu nikamtumia Smith shukurani za dhati. Baada ya kukisoma kitabu na kukifahamu nilimwandikia barua nyingine ambapo ndani yake nilimwambia:

“Mungu ameyapokea maombi yako na amenipa baraka nyingi kwa kitabu hiki lakini hata hivyo kinaenda kinyume na kubatilisha yale unayosema. Pindi tulipojadiliana ulisema kadha wakati kwenye kitabu nimekuta kadha ilihali ni Injili. Injili inaafikiana na Qur-aan juu ya umoja wa Allaah na uanadamu wa kawaida wa ´Iysaa. Kuna dalili nyingi na za wazi juu ya hilo.”

Nikamtajia dalili saba. Hapo ndipo ilikuwa mara ya mwisho kuwasiliana.

Naweza kushuhudia ya kwamba padiri yule kijana alikuwa ni mkweli[3] katika misionari yake na alikuwa na hamasa za hali ya juu. Kila nilipokuwa namwambia kitu fulani hakiko sawa ananambia kuwa akili ni pungufu na kwamba Allaah ni mkamilifu na kwamba anajua tusiyoyajua. Kabla ya kupata kitabu nilimtembelea kwenye shule yake ya misionari. Nikaja kujua kuwa hali nyama kabisa. Alikuwa akimwambia mpishi wake ampikie chakula cha mboga mboga na ampikie nyama mke na mtoto wake wa kiume. Nikamuuliza juu ya hilo. Akanambia kuwa anajaribu kuwaingiza wahindi kwenye ukristo kwa kutokula nyama. Wanachukia vibaya sana kula nyama. Akanambia kuwa ameacha kula nyama kwa ajili ya Masihi. Nikamwambia kuwa hawamuoni pindi anapokuwa nyumbani kwake. Akanambia ya kwamba hawezi kuwadanganya na kuwaambia kuwa hali nyama ilihali anaila. Kwa ajili hiyo ndio maana uhubiri wake uliwaathiri. Nilimwona yeye akiwa pamoja na wanaume thelathini na wake zao na watoto wakifanya yale anayoyasema. Aliwaamrisha wajenge kabisa. Wakajenga mikono yao pamoja na kuwa na kuwa walikuwa mafakiri. Hayo ni tofauti na yule padiri aliyekuwa akinifunza kingereza Lucknow. Hakuna aliyekuwa akimuamini – yeye mwenyewe alikuwa haamini. Ukweli[4] ndio ufunguo wa mafanikio, hata katika batili.

[1] Taaliki mbalimbali juu ya Matayo ya Injili.

[2] Tazama https://en.wikipedia.org/wiki/Shakib_Arslan

[3] Mukhlisw.

[4] Ikhlasw.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Taqiyy-ud-Diyn al-Hilaaliy al-Maghribiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Baraahiyn al-Injiylyyah ´alaa anna ´Iysaa daakhil fiyl-´Ubuudiyyah wa la hadhdhwa lahu fiyl-Uluuhiyyah, uk. 28-30
  • Imechapishwa: 16/10/2016