Madhambi yanadhoofisha matashi ya moyo. Matashi ya madhambi yanapata nguvu na matashi ya tawbah yanadhoofika kidogo kidogo lakini kihakika. Hali inaweza kufikia mpaka kwamba matashi ya tawbah yakapotea ndani ya moyo kabisaaa. Lau ingekufa sehemu ya nusu yake, basi asingelitubia kwa Allaah. Anamuomba Allaah msamaha na kutubia kwa wingi tawbah ya waongo. Sambamba na hilo moyo wake umefungamana na maasi na huku ni mwenye kuazimia kutumbukia ndani yake pale tu atapopata fursa. Haya ni katika maradhi makubwa na moja ya sababu zinazopelekea kuangamiza kwa karibu.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 69
  • Imechapishwa: 07/01/2018