11. Kulazimiana sehemu iliyoko kati ya kona na mlango

38- Inafaa kwake yeye kulazimiana na sehemu iliyoko baina ya kona na mlango kwa njia ya kwamba mtu aweke pale kifua chake, uso wake na viganja vyake[1].

39- Twawaaf haina Dhikr maalum. Inafaa kwake yeye kusoma Qur-aan na Dhikr kile atachokitaka. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kufanya Twawaaf katika Nyumba ni kama swalah. Lakini Allaah amehalalisha ndani yake kuzungumza. Atakayezungumza basi asizungumze isipokuwa kheri tu.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

“Ndani yake fanyeni uchache wa maneno.”[2]

40- Haijuzu kutufu katika Ka´bah kwa aliye uchi au mwanamke aliye na hedhi. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hatufu katika Nyumba aliye uchi.”[3]

Vilevile (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia ´Aaishah pindi alipofika hali ya kuwa ni mwenye kufanya ´Umrah katika hajj ya kuaga:

“Fanya kila kama anavofanya mwenye kuhiji isipokuwa tu usitufu na wala usiswali mpaka utwaharike.”[4]

41- Atapomaliza ule mzunguko wa saba, atanifunika bega lake la kulia, ataenda sehemu ya kusimama Ibraahiym na atasoma:

وَاتَّخِذُوا مِن مَّقَامِ إِبْرَاهِيمَ مُصَلًّى

“Fanyeni mahali pa kusimama Ibraahiym kuwa ni sehemu ya kuswalia.”[5]

42- Ataswali Rak´ah mbili baina ya sehemu ya kusimama pa Ibraahiym na Ka´bah.

43- Atasoma katika Rak´ah mbili hizo:

قُلْ يَا أَيُّهَا الْكَافِرُونَ

“Enyi makafiri!”[6]

na:

قُلْ هُوَ اللَّـهُ أَحَدٌ

“Sema: “Yeye ni Allaah Mmoja pekee.”[7]

44- Mtu hatakiwi kupita mbele ya mwenye kuswali na wala asimwache yeyote kupita mbele yake. Kwa sababu zile Hadiyth zenye kukataza kitendo hicho ni zenye kuenea. Upande mwingine haikuthibiti kuvuliwa msikiti Mtakatifu au Makkah yote[8].

45- Atapomaliza kuswali mtu anatakiwa kwenda katika zamzam na atakunywa kutoka hapo na atajimiminia kichwani mwake. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Maji ya zamzam ni kwa ile nia aliyonywewa.”[9]

Vilevile amesema tena:

“Hakika ni yenye baraka. Ni chakula chenye kushibisha na ni ponyo kwa maradhi.”[10]

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Maji bora zaidi ulimwenguni ni zamzam. Ni chakula chenye kushibisha na ni ponyo kwa maradhi.”[11]

46- Kisha mtu atarudi katika jiwe jeusi na aseme “Allaahu Akbar” na ataigusa kwa upambanuzi uliyopambanuliwa.

[1] Haya yamepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia njia mbili. Kwa pamoja zinakuwa nzuri (Hasan). Ni jambo linakuwa na nguvu zaidi kwa vile imethibiti kwamba Maswahabah wengi walifanya hivo. Miongoni mwao ni pamoja vilevile na Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Sehemu hii mtu anatakiwa kulazimiana nayo; baina ya kona na mlango.”

Vilevile imesihi kutoka kwa ´Urwah bin az-Zubayr kwamba alifanya hivo. Yote haya yametajwa katika “al-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (2138).  Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema katika “al-Mansik” yake:

“Akitaka kuiendea sehemu hiyo – nayo ni sehemu iliyoko kati ya jiwe jeusi na mlango wa Ka´bah – aweke juu yake kifua chake, uso wake na viganja vyake na amuombe Allaah haja zake, afanye hivo. Inafaa kwake yeye kufanya hivo kabla ya Twawaaf-ul-Wadaa´ [Twawaaf ya kuaga]. Hakuna tofauti baina ya mtu kufanya jambo hili katika hali ya kuaga au katika hali nyingine. Maswahabah walikuwa wakifanya hivo wakati wanapoingia Makkah… Hata hivyo lililo bora ni yeye kusimama karibu na mlango na kuomba pasi na kulazimiana na Nyumba. Akigeuka kwa ajili ya kwenda hatosimama, hatogeuka na wala hatorudi kinyumenyume.” (Uk. 387)

[2] Ameipokea at-Tirmidhiy na wengineo. Upokezi mwingine umepokelewa na at-Twabaraaniy na wengine. Hadiyth ni Swahiyh, kama nilivyohakiki hilo katika ”al-Irwaa’” (21). Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Hakuna Dhikr yoyote maalum iliyopokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba aliamrisha, alisoma au alifunza. Bali mtu ataomba du´aa zote zilizowekwa katika Shari´ah. Yale yanayofanywa na baadhi ya watu ambapo wanaomba du´aa maalum chini ya mfereji wa paa na mfano wake hayana msingi wowote.”

[3] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka katika Hadiyth ya Abu Hurayrah. Vilevile at-Tirmidhiy ameipokea kutoka kwa ´Aliy na Ibn ´Abbaas. Imetajwa katika ”al-Irwaa’” (1102).

[4] Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim kutoka kwa ´Aaishah. al-Bukhaariy ameipokea pia kutoka kwa Jaabir. Ziada ni yake na imetajwa katika marejeo yaliyotangulia (191).

[5] 02:125

[6] 109:01

[7] 111:01

[8] Rejea katika “chanzo”, uk. 21, 23 na 135.

[9] Hadiyth ni Swahiyh kama ilivyosemwa na maimamu wengi. Nimeitaja na kuzungumzia njia zake katika ”Irwaa’- ul-Ghaliyl” (11y23). Moja katika hizo imetajwa katika ”as-Swahiyhah” (883).

[10] Hadiyth ni Swahiyh. Imepokelewa na Abu Daawuud at-Twayaalisiy na wengineo.  Imetajwa katika ”as-Swahiyhah” chini ya Hadiyth 1056.

[11] Ameipokea adh-Dhwiyaa’ katika ”al-Mukhtaarah” na wengineo. Imetajwa katika marejeo yaliyotangulia (1056).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 22-23
  • Imechapishwa: 08/07/2018