11. Kufunguliwa na kufungwa kwa kifua

… na akavifungua vifua vyao kwa ajili ya ukumbusho – Pindi Allaah anapotaka kumwongoza mtu basi hukifungua kifua chake ambapo akakubali wito kwa Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

فَمَن يُرِدِ اللَّـهُ أَن يَهْدِيَهُ يَشْرَحْ صَدْرَهُ لِلْإِسْلَامِ

“Basi yule ambaye Allaah anataka kumwongoza, humfungulia kifua chake kwa Uislamu… “

Anakuwa ni mwenye kukubali na mwenye shauku na hivyo Allaah anakifungua kifua chake juu ya Uislamu. Huu ni utashi wa kilimwengu:

وَمَن يُرِدْ أَن يُضِلَّهُ يَجْعَلْ صَدْرَهُ ضَيِّقًا حَرَجًا

“… na yule ambaye anataka kumpotoa, basi hufanya kifua chake kuwa na dhiki chenye uzito.”[1]

Huu pia ni utashi wa kilimwengu. Anakuwa si mwenye kukubali kitu. Hapendi kheri. Anakimbia mbali na kheri na watu wa kheri:

كَأَنَّمَا يَصَّعَّدُ فِي السَّمَاءِ

“… kama kwamba anapanda kwa tabu mbinguni.”[2]

Kifua chake kinakuwa chenye dhiki. Wanahisi dhiki kutokamana na haki, ulinganizi kwa Allaah, usomwaji wa Qur-aan, mawaidha na ukumbusho. Kwa sababu Allaah amefanya vifua vyao kuwa vyenye dhiki kwa ajili ya kuwaadhibu kutokana na kupuuzia kwao. Hivyo Allaah anawanyima uongofu.

[1] 06:125

[2] 6:125

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 16
  • Imechapishwa: 05/07/2021