Kila mtu ambaye anazua kitu ambacho anajikurubisha kwacho mbele ya Mola Wake – kinachohusiana na imani au matendo ya kimaneno au kivitendo – basi ni mpotevu. Dalili ya hilo ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Kila Bid´ah ni upotevu.”[1]

´Kila` hii ni yenye kuenea na haivui kitu kabisa. Kila Bid´ah ndani ya dini ya Allaah ni upotevu na ndani yake hakuna chochote kinachohusiana na haki. Kwani Allaah (Ta´ala) amesema:

فَمَاذَا بَعْدَ الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ

“Kuna nini baada ya haki isipokuwa upotofu? Basi vipi mnageuzwa?”[2]

[1] Muslim (867).

[2] 10:32

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah fiy-´Aqiydah wal-´Amal, uk. 23
  • Imechapishwa: 23/07/2019