11. Iyaas bin Mu´aadh anaingia katika Uislamu

Allaah alifanya wanusuraji, Answaar wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwenye kabila la al-Aws na al-Khazraj walikuwa wakisikia kutoka mabwana zao wa kiyahudi al-Madiynah wanapozungumza juu ya kwamba kuna Mtume ametumwa katika zama hizi. Walipokuwa wanapogombana wanawatishia na kusema:

“Sisi pamoja na yeye tutakuueni kama walivyouawa kina ´Aad na Iram.”

Wanusuraji walikuwa wakihiji Ka´bah kama walivyokuwa wakihiji waarabu wengine wote. Mayahudi walikuwa hawafanyi hivo. Wakati Answaar walipomuona jinsi Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anavyowalingania watu katika dini ya Allaah (Ta´ala) na alama yenye kuonesha ukweli wake wakasema:

“Kwa jina la Allaah! Huyu ndiye ambaye mayahudi walikuwa wakikutishieni naye! Wasikutangulieni kwake kabla yenu.”

Suwayd bin as-Swaamit, ndugu wa Banuu ´Amr bin ´Awf bin al-Aws, alikuwa amefika Makkah. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamlingania, lakini hakuitikia na badala yake akasafiri kurudi al-Madiynah na akauawa katika moja ya vita vyao. Suwayd huyu alikuwa ni binadamu wa ´Abdul-Muttwab. Baada ya hapo Abuul-Haysar Anas bin Raafi´ akafika Makkah akiwa na kundi la vijana kutoka katika kabila la Banuu ´Abdil-Ashhal wakitafuta washirika. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawalingania katika Uislamu ambapo kijana wao mmoja kwa jina Iyaas bin Mu´aadh akasema:

“Watu wangu! Ninaapa kwa Allaah ya kwamba hili ni bora kuliko yale tuliyoyajia kwa ajili yake.”

Abuul-Haysar akampa kibao na kumkaripia na akawa amekaa kimya. Hawakufanikiwa kutimiza washirika wao na wakarudi katika mji wao al-Madiynah. Inasemekana kuwa Iyaas bin Mu´aadh alikufa akiwa ni muislamu.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Kathiyr ad-Dimashqiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fusuwl fiy Siyrat-ir-Rasuwl, uk. 28-29
  • Imechapishwa: 18/03/2017