1- Inafaa kwa msafiri kula katika mwezi wa Ramadhaan katika kile kipindi cha safari yake kisha alipe baadaye alipe zile siku alizokula. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini, basi atimize idadi katika masiku mengine.”[1]

2- Msafiri aliyefunga katika mwezi wa Ramadhaan amekhiyarishwa kati ya kufunga na kula. Hata hivyo akila atatakiwa kulipa. Hayo ni kutokana na yale yaliyothibiti kwa al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesimulia kuwa Hamzah bin ´Imraan al-Aslamiy alisema kumwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Je, nifunge nikiwa safarini?” – mtu huyu alikuwa ni mwenye kufunga sana – akamjibu: “Ukitaka funga na ukitaka kula.”[2]

[1] 02:185

[2] al-Bukhaariy (1943) na Muslim (1121).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 17
  • Imechapishwa: 18/04/2019