Maana ya hedhi kilugha ni kutirizika.

Maana ya hedhi Kishari´ah ni damu inayotoka katikati ya mfuko wa uzazi wa mwanamke katika nyakati maalumu pasi na maradhi na kufikwa na jambo. Ni jambo ambalo Allaah amewaumbia wanawake wa Aadam. Allaah ameiumbia kwenye mfuko wa uzazi wa mwanamke ili iwe ni chakula cha mtoto ndani ya tumbo wakati wa ujauzito kisha inageuka kuwa maziwa baada ya kuzaa kwake. Mwanamke akiwa hana mimba wala hanyonyeshi, basi damu hiyo inabaki haina mahali pa kutoka na hivyo inakuwa ni yenye kutoka katika nyakati maalumu. Damu hiyo inatambulika kama ada au hedhi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat , uk. 27
  • Imechapishwa: 24/10/2019