11. Haijuzu kwa mwanamke kutoka kwenda mahala pa kuswalia bila ya mavazi ya juu


2- Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoamrisha wanawake kutoka kwenda mahala pa kuswalia Idi, alisema:

“Ee Mtume wa Allaah! Baadhi yetu hawana mavazi ya juu ya kutokea?” Akasema: “Dada yake amvishe moja katika mavazi yake ya juu.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy, Muslim na wengine.

Hadiyth hii dalili inayoonyesha kuwa iliwa ni katika mazowea ya wanawake wa Maswahabah kutotoka isipokuwa kwa mavazi ya juu na ikiwa hana hatoki. Ndio maana (Radhiya Allaahu ´anhunn) wakamtajia kizuizi hichi pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipowaamrisha kutoka kwenda mahala pa kuswalia Idi wakati wa Idi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawatatulia tatizo hili, waazime kutoka kwa kina dada. Pamoja na hivyo hakuwaacha wakatoka bila ya mavazi ya juu hata kama imewekwa katika Shari´ah na kuamrishwa kwa wanaume na wanawake kutoka na kwenda mahapa pa kuswalia Idi. Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwaacha wakatoka bila ya mavazi ya juu kwa kitu ambacho kimeamrishwa, ni vipi angeliwaacha wakatoka bila ya mavazi ya juu na kwenda kwa kitu ambacho hakikuamrishwa wala kisichokuwa na haja kama mfano wa masoko na kuchanganyika na wanaume na kuangalia mambo yasiyokuwa na faida. Kuamrishwa kwa mavazi ya juu ni jambo lenye kutolea dalili kuonyesha kuwa ni wajibu kwa mwanamke kujifunika na Allaah ndiye anajau zaidi.

[1] al-Bukhaariy (324) na Muslim (890).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hijaab, uk. 15-16
  • Imechapishwa: 26/03/2017