59- al-´Irbaadhw bin Saariyah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimekuacheni katika mfano wa weupe[1]; usiku wake ni kama mchana wake. Hakuna atakayepotea nao isipokuwa mwangamivu.”[2]

Ameipokea Ibn Abiy ´Aaswim katika ”as-Sunah”[3] kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[1] Mila na hoja ya wazi ambayo haikubali shubuha kabisa. Hali yake wakati inashambuliwa na shubuha ni kama hali yake wakati shubuha inafichuliwa na kuzuiwa. Ishara ya hayo iko katika maneno yake ”usiku wake ni kama mchana wake”.

[2] Swahiyh.

[3] Kadhalika Ahmad, Ibn Maajah na al-Haakim katika baadhi yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/131)
  • Imechapishwa: 27/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy