11. Hadiyth “Miongoni mwa matendo na mema yanayoambatana na muumini baada ya kufa kwake… “


77- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Miongoni mwa matendo na mema yanayoambatana na muumini baada ya kufa kwake ni elimu aliyoifunza au aliyoieneza, mtoto mwema aliyemwacha nyuma yake, Mushaf aliouacha katika mirathi, msikiti aliyoujenga, nyumba aliyoijenga kwa sababu ya wapita njia (wasafiri), mfereji aliochimba au swadaqah alioitoa kutoka katika mali yake wakati akiwa na afya njema na wakati bado akiishi – haya ndio yanayoambatana na mtu baada ya kufa kwake.”[1]

Ameipokea Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi nzuri, al-Bayhaqiy na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” kwa muundo wenye kusema:

“… mfereji aliochimba… “

Hakutaja Mushaf.

[1] Nzuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/142-143)
  • Imechapishwa: 24/09/2018
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy