11. Hadiyth “Hakuna miongoni mwenu mtu ambaye atatayarisha maji kwa ajili ya kutawadha… “

186 – ´Amr bin ´Abasah as-Sulamiy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kipindi cha kale kabla ya kuja Uislamu nilikuwa nikiona kuwa watu wako juu ya upotofu na kwamba hawako juu ya chochote kwa sababu walikuwa wakiabudia masanamu. Ndipo nikasikia kuhusu mtu aliyeko Makkah ambaye alikuwa anaelezea khabari mbalimbali, nikaketi juu ya kipando changu na nikamwendea. Tahamaki alikuwa ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)… Nikasema: “Ee Nabii wa Allaah! Nihadithie kuhusu wudhuu´.” Akasema: “Hakuna miongoni mwenu mtu ambaye atatayarisha maji kwa ajili ya kutawadha ambapo akasukutua, akapalizia na kuyapenga isipokuwa makosa ya usoni mwake huondoka kwenye ndevu zake pamoja na yale maji. Kisha akaosha mikono yake mpaka kwenye visugudi isipokuwa makosa ya mikononi mwake huondoka katika ncha za vidole vyake kwa yale maji. Kisha akapangusa kichwa chake isipokuwa makosa ya kichwa chake hutoka katika nywele zake pamoja na yale maji. Kisha akaosha miguu yake kukiwemo vifundo viwili vya miguu isipokuwa makosa ya miguu yake yanaondoka kwenye vidole vyake kwa yale maji. Akisimama na kuswali ambapo akamuhimidi Allaah (Ta´ala), akamsifu na akamtukuza kwa vile anavostahiki na akaufaraghisha moyo wake kwa Allaah (Ta´ala), isipokuwa ataondoka kutoka katika hiyo swalah yake kama ile siku mama yake aliyomzaa.”[1]

Ameipokea Muslim.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/192)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy