11. Hadiyth “Atakayejitwaharisha na kuoga, akawa karibu na mapema… “

693- ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayejitwaharisha na kuoga, akawa karibu na mapema, akakaribia na kusikiliza, basi hulipwa kwa kila hatua moja anayopiga ujira wa swawm ya mwaka mzima na kisimamo chake cha usiku.”[1]

Ameipokea Ahmad na wanaume wake ni Swahiyh[2].

[1] Swahiyh.

[2] Katika mlolongo wa wapokezi amekuja ´Uthmaan ash-Shaamiy ambaye anaitwa ´Uthmaan bin Abiy Sawdah al-Maqdisiy. Hakupokea katika ”as-Swahiyh”. al-Bukhaariy amepokea kwake katika ”al-Adab al-Mufrad” na sio katika ”as-Swahiyh”. Hata hivyo alikuwa ni mwaminifu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/435)
  • Imechapishwa: 31/03/2017