48- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema wakati anapoingia Msikitini:

بِسْمِ اللهِ اللَّهُمَّ صَلِّ عَلىَ مُحَمَّدٍ

“Kwa jina la Allaah. Allaah! Mtaje Allaah katika ulimwengu wa juu.”

Wakati anapotoka alikuwa akisema:

بِسْمِ اللهِ اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ

“Kwa jina la Allaah. Ee Allaah! Mtaje Allaah katika ulimwengu wa juu.”

49- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu anapoingia Msikitini amswalie Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aseme:

اللهُمَّ افْتَحْ لِي أَبْوَابَ رَحْمَتِكَ

“Allaah! Nifungulie milango ya Rahmah Zako.”

Wakati anapotoka aseme:

اللَّهُمَّ إِنِّي أَسْأَلُكَ مِنْ فَضْلِكَ

“Allaah! Ninakuomba fadhila Zako.”

Katika upokezi mwingine asalimu wakati wa kutoka.

50- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati akiingia Msikitini alikuwa akisema:

أَعُوذُ باللهِ الْعَظِيم وَبِوَجْهِهِ الْكَرِيمِ وَبِسُلْطَانِهِ الْقَدِيمِ مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ

“Najikinga na Allaah, Mtukufu, na kwa Uso Wake Mtukufu na kwa utawala Wake wa milele kutokana na Shaytwaan Aliyewekwa mbali na Rahmah za Allaah.”

Akasema:

”Akisema hivo Shaytwaan husema: ”Amehifadhiwa na mimi siku iliobaki.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 46-47
  • Imechapishwa: 21/03/2017