11. Dalili ya kwamba Allaah hakutuacha bure pasi na malengo yoyote

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

… na gakutuacha bure tu pasi na malengo…

MAELEZO

Huu ndio uhakika wa mambo ambao unafahamishwa na dalili za Qur-aan na Sunnah na dalili za kiakili. Kuhusu dalili za Qur-aan na Sunnah ni kwa mfano maneno Yake (Ta´ala):

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ

“Je, mlidhania kwamba Sisi tulikuumbeni bila kusudio na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa? Basi ametukuka Allaah, Mfalme wa haki, hapana mungu wa haki isipokuwa Yeye! Mola wa ‘Arshi tukufu.” (al-Mu´minuun 23 : 115-116)

أَيَحْسَبُ الْإِنسَانُ أَن يُتْرَكَ سُدًى أَلَمْ يَكُ نُطْفَةً مِّن مَّنِيٍّ يُمْنَىٰ ثُمَّ كَانَ عَلَقَةً فَخَلَقَ فَسَوَّىٰ فَجَعَلَ مِنْهُ الزَّوْجَيْنِ الذَّكَرَ وَالْأُنثَىٰ أَلَيْسَ ذَٰلِكَ بِقَادِرٍ عَلَىٰ أَن يُحْيِيَ الْمَوْتَىٰ

”Je, anadhani mtu ataachwa bure bila lengo? Kwani hakuwa tone kutokana na manii lilotonwa, kisha akawa pande la damu, akamuumba na akamsawazisha ambapo akamjaalia jozi, dume na jike? Je, hivyo Muumbaji huyo hakuwa ni muweza wa kuhuisha wafu?” (al-Qiyaamah 75 : 36-40)

Kuhusu dalili za kiakili ni kwamba haistahiki kwa hekima ya Allaah (´Azza wa Jall) mtu akaishi na kustarehe kama wanyama wanavyostarehe, halafu hatimaye akafa pasi na kufufuliwa wala kuhesabiwa. Ni upuuzi mtupu. Ni jambo lisiloingia akilini Allaah akaumba kiumbe hichi, akakitumia Mtume na akatuhalalishia damu kwa kupigana na wale wapinzani na wanaoenda kinyume na Mitume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam), kisha natija isiwe ni chochote. Hili ni jambo lisilowezekana kabisa kutokana na hekima ya Allaah (´Azza wa Jall).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 18/05/2020