11. Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal wataingia Motoni


Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

na upotevu na watu wake ni Motoni.

Upotebu na wapotevu ni wataingia Motoni ima kutokana na kufuru yao au maasi yao. Bid´ah zote haziko katika kiwango kimoja. Kuna ambazo ni kufuru na mwenye nazo atadumishwa Motoni milele. Mfano wazo ni kama kuwataka uokozi maiti, kuwaomba maiti, kuchinja kwa ajili ya asiyekuwa Allaah na kuweka nadhiri kwa asiyekuwa Allaah. Hizi mfano wa Bid´ah za kikafiri. Mfano mwingine ni kama kukanusha majina na sifa za Allaah kama wanavyofanya Jahmiyyah. Hii ni kufuru. Wamemsifu Allaah kutokuwa na majina na sifa. Katika hali hiyo inakuwa ni kitu kisichokuwepo. Kitu kilichopo ni lazima kiwe na sifa. Kitu kisichokuwepo ndio hakina sifa. Kwa ajili hiyo ndio maana maimamu wamewakufurisha Jahmiyyah. Ukiongezea juu ya hilo wamesema kuwa Qur-aan imeumbwa. Wameifanya Qur-aan – ambayo ni maneno ya Allaah, Wahy na uteremsho Wake – kwamba imeumbwa kama viumbe wengine na kwamba Allaah. Hivyo ni kitu kisichokuwa na uhai.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 21
  • Imechapishwa: 11/10/2017