La tisa: Aayah tukufu tunapata faida nyingine kwamba, yule mwenye kumtukana Allaah, Mtume wake, Kitabu Chake au Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni mamoja akiwa amekusudia kweli, anafanya mzaha au anafanya mchezo. Kwa sababu jambo hili ndani yake hakuna mzaha wala mchezo. Mzaha na mchezo haijuzu katika jambo hili. Mwenye kumtukana Allaah, Mtume, Qur-aan, Maswahabah au wale wanachuoni wanaowafuata, hakika matishio haya makali yanamgusa na anatoka katika dini na anaritadi japokuwa atakuwa ni mwenye kufanya mzaha tu. Kwa sababu wale watu ambao waliteremkiwa na Aayah walisema:

إِنَّمَا كُنَّا نَخُوضُ وَنَلْعَبُ

“Hakika tulikuwa tunaporoja na tunacheza.” (at-Tawbah 09:65-66)

Pamona na hivyo Allaah hakukubali udhuru wao. Bali alisema:

قُلْ أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

”Sema: ”Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake? Hivyo msitoe udhuru, kwani mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (at-Tawbah 09:66)

Ameininginiza hukumu kwa kule kufanya mzaha. Hakuna mzaha wala mchezo kumfanyia Allaah, Mtume wake au Aayah Zake. Ni wajibu kuyaheshimu mambo haya na kutoyafanyia mzaha wala mchezo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 139
  • Imechapishwa: 27/12/2018