109. al-Qummiy upotoshaji wake wa kwanza wa al-Maa-idah


al-Qummiy amesema:

“al-Husayn bin Muhammad bin ´Aamir ametukhabarisha, kutoka kwa al-Ma´laa bin Muhammad al-Baswriy, kutoka kwa Ibn Abiy ´Umayr, kutoka kwa Abu Ja´far yule wa pili ambaye amesema kuhusiana na maneno Yake:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَوْفُوا بِالْعُقُودِ

“Enyi walioamini! Timizeni mikataba.”[1]

Mtume wa Allaah alifunga fungamano kumi juu ya ukhaliyfah wa ´Aliy. Kisha Allaah akateremsha:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ أَوْفُواْ بِالْعُقُودِ التي عقدت عليكم لأمير المؤمنين

“Enyi walioamini! Timizeni mikataba iliyofungwa juu yenu kuhusu kiongozi wa waumini.[2]

Tazama namna ambavyo Baatwiniy huyu anavyomzulia uongo Allaah (´Azza wa Jall)? Mwishoni mwa Aayah akaongeza:

التي عقدت عليكم لأمير المؤمنين

“… iliyofungwa juu yenu kuhusu kiongozi wa waumini.”

halafu anamnasibishia uongo huu Abu Ja´far yule wa pili – Allaah amemtakasa kutokamana na uongo na ukafiri huu!

Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wamewasifu Muhaajiruun na Answaar kutokamana na imani yao ya kweli, Ikhlaasw yao, wema wao wa kukabiliana na mitihani, subira yao juu ya maudhi na mabalaa kutoka kwa maadui zao, kupambana kwao katika njia ya Allaah ili kulinyanyua neno la Allaah, kujitolea kwao kwa hali ya juu katika mapambano, utiifu wao usiokuwa na mfano na kumpenda kwao zaidi kuliko walivyokuwa wanazipenda nafsi zao wenyewe, watoto wao, baba zao na mali zao. Waliwaua na wakapigana na ndugu zao kukiwemo baba zao na watoto wao. Walikuwa wakimtii kwa dhahiri na kwa siri. Kiasi cha kwamba wakati Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomteua Usamaah bin Zayd kuwa ndiye kiongozi wao, ambaye ndiye alikuwa na umri mdogo na nafasi ya chini katika wao, wakakubali kwa kuridhia. Ni jambo lililokuwa linajulikana kwao na hakuna mtu mwengine isipokuwa mbishi na mjeuri ndiye awezaye kupinga.

Ni vipi basi mtu anaweza kufikiria kuwa mabwana hawa watukufu walivunja ahadi hata kama ingelikuwa kati yao wao na makafiri au watu wakubwa kabisa wasiokuwa na maana yoyote? Ni nani anayekubali na kuhakikisha dhambi na uzushi wa Baatwiniy huyu ambaye anadai kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifunga fungamano na wao kuhusu ukhaliyfah wa ´
Aliy ambapo baadaye wakaivunja? Ninaapa kwa Allaah mtu hawezi hata kufikiria kuvunjwa kwa ahadi moja juu ya kitu kidogo sembuse ahadi kumi tena kwa kitu kikubwa kama vile ukhaliyfah! Ni nani katika wao aliyevunja kiapo cha utifu cha Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan ili kukubaliwe kuvunjwa kwa ahadi kumi za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Wao ndio walikuwa watu wajuzi zaidi na ndio walikuwa watu wajuzi zaidi juu ya ukhatari wa kuvunjwa kwa ahadi kwa watu walio chini yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) – tusemeje juu ya kuvunjwa kiapo chake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Ni kwa nini ´Aliy akiwa pamoja na Banuu Haashim alikula kiapo cha usikivu na utiifu kwa Abu Bakr na ´Umar, na baada ya hapo pia ´Uthmaan akiwa pamoja na al-Hasan na al-Husayn baada ya kuwa watuwazima, ikiwa kweli aliahidiwa ahadi kumi?

Ni kwa nini alikuwa akiswali nyuma ya maimamu hawa, akihiji pamoja nao, akifunga pale wanapofunga na akiacha kufunga pale wanapoacha kufunga, akiikaa katika vikao vya mashauriano yao na akitoa mtazamo wake? Ni kwa nini yeye na Banuu Haashim, al-Hasan na al-Husayn walikuwa wakichukua hadi zao za zawadi na ngawira? Ni kwa nini yeye na al-´Abbaas walienda kwa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ili awahukumu?

Je, yote haya hayafahamishi uongo wa Baatwiniyyah Raafidhwah na kwamba wanachotaka ni kuzalisha uadui kati ya ´Aliy na ndugu zake na kuzua ukhaliyfah, uongozi, ahadi na fungamano? Halafu wanayatumia hayo kwa ajili ya kuwakufurisha Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Enyi waongo! Hivi kweli Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikokoteza juu ya kuwapa utawala watu wa nyumbani kwake kufikia kiwango chote hichi? Ni wapi kulifungwa fungamano hizi kumi? Ni Qumm au Najaaf? Ni katika zama zipi zilifungwa ahadi na fungamano hizi?

Allaah azijaze mbaya nyuso za maadui wa Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)! Lau ´Aliy angelikutana na waongo hawa Baatwiniyyah na akaweza kuwatokomeza, basi angeliwasambaratisha kama alivyowasabaratisha wahenga wao.

[1] 05:01

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/160).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 156-157
  • Imechapishwa: 22/04/2018