Iwapo mtu au kipenzi na mtu wake wa karibu atapofikwa na kitu katika yale Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyozingatia kuwa ni kufa shahidi basi ni shahidi. Kuna sampuli tatu za kuwa shahidi:

1- Kufa shahidi duniani na Aakhirah. Ni yule mwenye kuuawa katika uwanja wa vita hali ya kumtakasia nia Allaah.

2- Kuwa shahidi katika dunia hii. Ni yule mwenye kuuawa katika uwanja wa vita kwa kujionyesha.

3- Kufa shahidi Aakhirah. Ni yule ambaye Shari´ah imethibitisha kuwa ni shahidi bila ya kufanyiwa hukumu za shahidi hapa duniani. Kwa mfano wa mwenye kuzama, mwenye kuungua mpaka akafa, mwenye kufa kwa maradhi ya pafu na wengineo[1].

[1] Tazama mlango wa 106.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 229
  • Imechapishwa: 20/12/2016