108. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa kumi na mbili wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema:

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا

“Hakuna yeyote katika Ah-ul-Kitaab isipokuwa atamuamini kabla ya kufa kwake na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”[1]

“al-Haarith bin al-Mughiyrah amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema: “Ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”[2]

Kisha akasema:

“al-Mufadhdhwalah bin Muhammad amesema: Nilimuuliza Abu ´Abdillaah kuhusiana na Aayah:

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا

“Hakuna yeyote katika Ah-ul-Kitaab isipokuwa atamuamini kabla ya kufa kwake na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”

ambapo akajibu: “Hii imeteremka kwa ajili yetu tu. Hakuna mtu kutoka katika kizazi cha Faatwimah anayekufa na kutoka katika dunia hii isipokuwa anakubali uongozi wa imamu kama ambavyo wana wa Ya´quub walvyokiri kwa Yuusuf na kusema:

تَاللَّـهِ لَقَدْ آثَرَكَ اللَّـهُ عَلَيْنَا وَإِن كُنَّا لَخَاطِئِينَ

 “Tunaapa kwa Allaah! Hakika Allaah amekupendelea kuliko sisi nasi bila shaka tulikuwa wakosa.”[3]

Mhakiki amerejesha kwa “al-Bihaar”, “as-Swaafiy” na “al-Burhaan” na kuweka taaliki kwa kusema:

“Amesema katika “al-Faydhw”: “Watu wa kitabu wanaokusudiwa hapa ni kizazi cha Faatwimah kutokana na pale Allaah (Subhaanah) aliposema:

ثُمَّ أَوْرَثْنَا الْكِتَابَ الَّذِينَ اصْطَفَيْنَا مِنْ عِبَادِنَا

“Kisha Tukawarithisha Kitabu wale tuliowateua miongoni mwa waja Wetu.”[4]

Wao ndio makusudio ya wateuliwa katika Aayah hii. Ibn Sinaan amepokea kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema kuhusu ´Iysaa:¨

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا

“Hakuna yeyote katika Ah-ul-Kitaab isipokuwa atamuamini kabla ya kufa kwake na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”

 “Imani ya watu wa Kitabu ni kumuamini Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

al-´Ayyaashiy amesema:

“al-Mashriqiy amepokea kutoka kwa watu wengi ya kwamba maneno Yake:

وَإِن مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ إِلَّا لَيُؤْمِنَنَّ بِهِ قَبْلَ مَوْتِهِ ۖ وَيَوْمَ الْقِيَامَةِ يَكُونُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا

“Hakuna yeyote katika Ah-ul-Kitaab isipokuwa atamuamini kabla ya kufa kwake na Siku ya Qiyaamah atakuwa shahidi juu yao.”

inakusudia Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna myahudi yeyote wala mnaswara kamwe anayekufa bila kutambua kuwa ni Mtume wa Allaah na kwamba walimkana.”[5]

Jaabir amepokea kutoka kwa Abu Ja´far ambaye amesema:

“Hakuna mtu wa dini yeyote anayekufa isipokuwa humuona Mtume wa Allaah na kiongozi wa waumini.”[6][7]

Mtu huyu na watu mfano wake wamejitwisha jukumu ya kwamba hawatotaja Aayah yoyote isipokuwa watahakikisha wameipotosha kwa mujibu wa upotevu wao. Aayah hii na ya kabla yake inamzungumzia ´Iysaa (´alayhis-Salaam). Maana ya Aayah ni kwamba hakuna Ahl-ul-Kitaab yeyote, sawa awe myahudi au mnaswara, atayekufa isipokuwa atamuamini ´Iysaa (´alayhis-Salaam). Hii ndio maana ya Aayah. Anakuja Baatwiniy huyu na kuanza kucheza na maana ya Aayah hii na kumsemea uongo Abu ´Abdillaah. Mara adanganye kuwa makusidio ni Mtume wa Allaah. Mara adanganye kuwa makusudio ni watu wa nyumba ya kwa Mtume. Wakati mwingine anasema kwamba hakuna mtu wa dini yeyote anayekufa isipokuwa humuona Mtume wa Allaah na kiongozi wa waumini. Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokamana na uongo huu na mgongano wa kipumbavu.

[1] 159

[2] Mhakiki amerejesha kwa “al-Bihaar” na “al-Burhaan”.

[3] 12:91

[4] 35:32

[5] Mhakiki amerejesha kwa “al-Bihaar” na “al-Burhaan”.

[6] Mhakiki amerejesha kwa “al-Bihaar” na “al-Burhaan”.

[7] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/283-284).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 154-155
  • Imechapishwa: 13/04/2018