Wanachuoni wamesema kuwa istihzai imegawanyika sehemu mbili:

1-  Mzaha wa wazi kwa maneno.

2- Mzaha kwa kuashiria.

Istihzai ya ishara ni kama kubebetua midomo au kupepesa macho yake hali ya kucheza shere wakati anaposikia Aayah au Hadiyth. Au vilevile akaashiria kwa ishara ambayo inaonyesha kudharau na kufanyia mchezo. Huku pia kunazingatiwa ni kucheza shere na kufanya istihzai. Haijalishi kitu hata kama hakutamka. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ

”Hakika wale waliofanya ukhalifu walikuwa [duniani] wakiwacheka wale walioamini. Na wanapowapitia [karibu yao], basi wanakonyezana.” (al-Mutwaffifiyn 83:29-30)

Ni lazima kwa muislamu kuzindukana juu ya jambo hili na ajiepushe na kuongea mambo mabaya na khaswakhaswa maneno juu ya mambo ya Shari´ah,  watu wa dini na wanachuoni. Anatakiwa kuuhifadhi ulimi wake. Amesema (Ta´ala):

مَّا يَلْفِظُ مِن قَوْلٍ إِلَّا لَدَيْهِ رَقِيبٌ عَتِيدٌ

”Hatamki kauli yeyote ile isipokuwa yuko karibu naye mwangalizi amejitayarisha kurekodi.” (Qaaf 50:18)

Huwezi kuijua haki na batili isipokuwa mpaka ujifunze elimu yenye manufaa. Allaah kateremsha Upambanuo, ambayo ni Qur-aan, ili ipambanue baina ya haki na batili. Amesema (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تَتَّقُوا اللَّـهَ يَجْعَل لَّكُمْ فُرْقَانًا

”Enyi mlioamini! Mkimcha Allaah atakupeni Kipambanuo.” (al-Anfaal 08:29)

Bi maana atajaalia ndani ya mioyo yenu kuwa nuru muweze kwayo kujua haki kutokamana na batili. Qur-aan ni upambanuo na  ni kipambanuo ambacho Allaah hujalia kwenye moyo wa muumini akawa anaweza kupambanua kati ya haki na batili. Kwa njia ya kwamba mambo yakawa hayamchanganyi, madai yenye kupotosha yakawa hayamuathiri wala shubuha zenye kupambwa. Lakini hata hivyo haya yanahitajia mtu kutilia umuhimu, kujifunza na mtu atahadhari kutokamana na wanafiki na mazanadiki waliopenyezwa kati ya safu za waislamu. Mtu asihudhurie majilisi zao. Ikitokea akahudhuria basi awe tayari kuwakemea, kuyasambaratisha maneno yao na kuraddi utata wao.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 138-139
  • Imechapishwa: 25/12/2018