107. Fadhilah za kumswalia Mtume (صلى الله عليه وسلم)

  Download

219-

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote mwenye kuniswalia mara moja, basi Allaah atamswalia mara kumi.”[1]

220-

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msilifanye kaburi langu kuwa ni mahali pa kutembelea mara kwa mara na niswalieni. Kwani hakika swalah zenu zinanifikia popote mlipo.”[2]

221-

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Bakhili ni yule nitakayetajwa mbele yake na asiniswalie.”[3]

222-

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah anao Malaika wanaozunguka ardhini wanaonifikishia salamu kutoka kwa Ummah wangu.”[4]

223-

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna yeyote anayeniswalia isipokuwa Allaah hunirudishia roho yangu ili niweze kumwitikia salamu.”[5]

[1] Muslim (01/288).

[2] Abu Daawuud (02/218) na Ahmad (02/367). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh  Abiy Daawuud” (02/383).

[3] at-Tirmidhiy (05/551) na wengineo. Tazama “Swahiyh al-Jaamiy’” (03/25). Tazama “Swahiyh-ut-Tirmidhiy” (03/177).

[4] an-Nasaa´iy (03/43) na al-Haakim (02/421). Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-un-Nasaa´iy”.

[5] abu Daawuud  (2041). Ni nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh Abiy Daawuud” (01/383).

  • Mhusika: Shaykh Sa´iyd bin ´Aliy bin Wahf al-Qahtwaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Huswn-ul-Muslim
  • Imechapishwa: 06/05/2020