Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”[1]

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Tegemea kwa Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kurehemu, ambaye anakuona wakati unaposimamama, na mageuko yako na wenye kusujudu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”[2]

MAELEZO

Hii ni dalili ya ngazi ya kwanza ya Ihsaan:

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”

Aayah imefahamisha kuwa Allaah yupamoja na watenda wema ambao ni wale wenye kumwabudu Allaah kama vile wanamuona. Allaah yupamoja nao upamoja maalum. Inahusiana na upamoja wa kuwanusuru, kuwatia nguvu na kuwaongoza.

Maneno Yake (Ta´ala):

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Tegemea kwa Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kurehemu, ambaye anakuona wakati unaposimamama, na mageuko yako na wenye kusujudu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”

Hii ni dalili ya ngazi ya pili. Hii ni dalili ya maneno yake:

“… basi hakika yeye anakuona.”

Tegemea – Bi maana yategemeze mambo yako.

Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kurehemu – Ni Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Wakati unaposimama – Unaposimama kwa ajili ya kufanya ´ibaadah na kuswali.

Na mageuko yako na wenye kusujudu – Anakuona ukiwa ni mwenye kurukuu na mwenye kusujudu. Anakuona katika hali zako zote za ´ibaadah ukiwa ni mwenye kusimama, kurukuu na kusujudu. Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) anakuona.

Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote – Allaah anasikia na anaona maneno yako (Subhaanahu wa Ta´ala).

[1] 16:128

[2] 26:217-220

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 225-226
  • Imechapishwa: 27/01/2021