Sahl bin Hunayf (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumuomba Allaah kikweli kufa shahidi, basi atafikia daraja ya mashahidi hata kama atakufa juu ya kitanda chake.”

Ameipokea Muslim. Muslim amepokea tena ya kupitia kwa Anas ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kumuomba Allaah kikweli kufa shahidi basi atafikia hata kama hatopatwa na hilo.”

at-Tirmidhiy amepokea na sahihisha muundo huo kupitia kwa Mu´aadh:

“Mwenye kuomba kufa katika njia ya Allaah akiwa ni mkweli kutoka moyoni mwake basi Allaah atampa ujira wa mashahidi.”

Ameipokea Imaam Ahmad.

Jaabir bin ´Atiyk (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallama) amesema:

“Kuna sampuli saba ya mashahidi mbali na kufa katika njia ya Allaah; mwenye kufa kwa ajili ya tauni, mwenye kufa kwa ugonjwa wa tumbo, mwenye kuzama, mwenye kuchomeka moto mpaka akafa, mwenye kufa kwa maradhi ya pafu, mwenye kufa kwa kuangukiwa na jengo na mwanamke mwenye kufa kwa Jum´.”

Ameipokea Imaam Ahmad, Abu Daawuud na an-Nasaa´iy.

Mwanamke mwenye kufa kwa Jum´ ni ima yule mwenye kufa akiwa na mimba au akiwa na nifasi, hivyo ndivyo walivyofasiri wanachuoni wengi na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 225-226
  • Imechapishwa: 17/12/2016