106. Allaah kawaridhia Maswahabah nao wameridhika Naye

Hali kadhalika wale wanaowatukana Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum). Watu hawa wanamkadhibisha Allaah (Jalla  wa ´Alaa). Kwani Allaah amewasifu Maswahabah katika Aayah nyingi. Amesema (Ta´ala):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ وَأَعَدَّ لَهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي تَحْتَهَا الْأَنْهَارُ

“Wale waliotangulia awali miongoni mwa Muhaajiruun na Answaar na wale waliowafuata kwa wema, Allaah ameridhika nao, nao wameridhika Naye na amewaandalia mabustani yapitayo chini yake mito.” (at-Tawbah 09:100)

Muhaajiruun na Answaar ndio Maswahabah walioridhiwa na Allaah. Upande mwingine hawa wanapinga haya na kwamba Maswahabah wamekufuru na kwamba eti hawakubaki katika Uislamu isipokuwa wane tu katika wao. Huku ni kumkadhibisha Allaah (´Azza wa Jall). Amesema (Jalla wa ´Alaa):

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّـهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖتَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ

“Muhammad ni Mtume wa Allaah. Na wale walio pamoja naye ni wakali zaidi dhidi ya makafiri wanahurumiana baina yao. Utawaona wakirukuu na wakisujudu wakitafuta fadhila na radhi kutoka kwa Allaah. Alama zao dhahiri zi katika nyuso zao kutokana na athari za sujudu.” (al-Fath 43:29)

Kisha wanasema kuwa Maswahabah ni makafiri? Allaha ametakasika. Wanawasema vibaya na kuwakufurisha wale ambao Allaah amewasifu. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

لِلْفُقَرَاءِ الْمُهَاجِرِينَ الَّذِينَ أُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأَمْوَالِهِمْ يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّـهِ وَرِضْوَانًا وَيَنصُرُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ ۚ أُولَـٰئِكَ هُمُ الصَّادِقُونَ

”[Na pia wapewe fungu la ngawira] kwa masikini Muhaajiruun ambao wametolewa kutoka majumbani mwao na [wakaacha] mali zao wanatafuta fadhila kutoka kwa Allaah na radhi  na wanamnusuru Allaah na Mtume Wake, hao ndio wakweli.” (al-Hashr 59:08)

Hawa ndio Muhaajiruun. Halafu akasema kuhusu Answaar:

وَالَّذِينَ تَبَوَّءُوا الدَّارَ وَالْإِيمَانَ مِن قَبْلِهِمْ يُحِبُّونَ مَنْ هَاجَرَ إِلَيْهِمْ وَلَا يَجِدُونَ فِي صُدُورِهِمْ حَاجَةً مِّمَّا أُوتُوا وَيُؤْثِرُونَ عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ وَلَوْ كَانَ بِهِمْ خَصَاصَةٌ ۚ وَمَن يُوقَ شُحَّ نَفْسِهِ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

”Wale waliokuwa na makazi [Madiynah] na wakawa na imani kabla yao wanawapenda wale waliohama kwao na wala hawapati kuhisi haja [husda] yoyote vifuani mwao kwa yale waliyopewa na wanawapendelea kuliko nafsi zao japokuwa wao wenyewe ni wahitaji. Na yeyote yule anayeepushwa na uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufaulu.” (al-Hashr 59:09)

Hawa ndio Answaar na hizi ndizo sifa zao. Kisha akasema:

وَالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ

”Wale waliokuja baada yao… ”

Bi maana baada ya Muhaajiruun na Answaar.

يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

”… husema: “Tusamehe na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala usijaalie katika nyoyo zetu mafundo kwa wale walioamini. Ee Mola wetu! Hakika Wewe ni Mwenye huruma, Mwenye kurehemu.” (al-Hashr 59:10)

Lakini mambo yanakuweje ikiwa wale waliokuja baada yao wanasema:

“Ee Allaah! Mlaani Abu Bakr na ´Umar, ´Aaishah mama wa waumini na fulani na fulani katika Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum)? Ipi hukumu yao mbele ya Allaah (Ta´ala)? Tunamuomba Allaah afya.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 136-137
  • Imechapishwa: 25/12/2018