106. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na tano wa an-Nisaa´


al-Qummiy amesema:

لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ

“Lakini Allaah anayashuhudia aliyoyateremsha kwako [kwamba] ameyateremsha kwa ujuzi Wake, na Malaika pia wanashuhudia. Na Allaah anatosheleza kuwa Mwenye kushuhudia yote.”[1]

Baba yangu amenihadithia, kutoka kwa Ibn Abiy ´Umayr, kutoka kwa Abu Baswiyr, kutoka kwa Abu ´Abdillaah ambaye amesema:

“Ukweli wa mambo imeteremshwa namna hii:

لَّـٰكِنِ اللَّـهُ يَشْهَدُ بِمَا أَنزَلَ إِلَيْكَ في علي ۖ أَنزَلَهُ بِعِلْمِهِ ۖ وَالْمَلَائِكَةُ يَشْهَدُونَ ۚ وَكَفَىٰ بِاللَّـهِ شَهِيدًا إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَصَدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ قَدْ ضَلُّوا ضَلَالًا بَعِيدًا  إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَظَلَمُوا آل محمد حقهم لَمْ يَكُنِ اللَّـهُ لِيَغْفِرَ لَهُمْ وَلَا لِيَهْدِيَهُمْ طَرِيقًا  إِلَّا طَرِيقَ جَهَنَّمَ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ وَكَانَ ذَٰلِكَ عَلَى اللَّـهِ يَسِيرًا

“Lakini Allaah anayashuhudia aliyoyateremsha kwako kuhusu ´Aliy [kwamba] ameyateremsha kwa ujuzi Wake, na Malaika pia wanashuhudia, na Allaah anatosheleza kuwa Mwenye kushuhudia. Hakika wale waliokufuru na wakazuia njia ya Allaah, hakika wamekwishapotea upotofu wa mbali.  Hakika wale waliokufuru na wakadhulumu haki ya kizazi cha Muhammad, haitokuwa kwa Allaah kuwasamehe wala kuwaongoza njia isipokuwa njia ya [Moto wa] Jahannam hali ya kuwa ni wenye kudumishwa humo milele. Na hayo kwa Allaah ni mepesi.”[2][3]

Raafidhwiy huyu katika kufasiri Aayah hizi amekusanya kati ya kumzulia Allaah uongo kwa kuongeza “kuhusu ´Aliy” na kuongeza pia “haki ya kizazi cha Muhamma”. Anamsemea Allaah uongo na kupotosha maana ya Aayah. Kwani makusudio ya Aayah ni kuthibitisha ujumbe wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah na Malaika wote wanashuhudia juu ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Mtume wa Allaah, jambo ambalo ni Radd kwa washirikina na mayahudi ambao wanakadhibisha ujumbe huu mkubwa ambao umekusanya kheri zote za duniani na Aakhirah na wenye kushinda ujumbe wote. Halafu anakuja Baatwiniy huyu na kuzikengeusha kwenda katika maana isiyokuwa na nafasi na wala isiyolingana na ujumbe huu uliobarikiwa. Kwa sababu ukengeushaji huu unapelekea kumkanusha Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba hakuwa ni mwenye kutumwa kutoka kwa Allaah ili kuwatoa watu kutoka katika giza kwenda katika nuru, isipokuwa alikuja kwa ajili ya kusimamisha utawala juu ya watu wa nyumbani kwake. Haya ndio malengo ya Baatwiniyyah hawa wanayotumia kwa ajili ya kutaka kuubomoa Uislamu, waislamu, kuwakufurisha na kuwahukumu ya kwamba wataingia Motoni milele na khaswa khaswa Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] 04:116

[2] 04:116-119

[3] Tafsiyr al-Qummiy (1/159))

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 152-153
  • Imechapishwa: 13/04/2018