Swali 105: Wakati fulani namfanyia Twawaaf mmoja katika jamaa zangu, wazazi wangu au babu zangu waliofariki. Ni ipi hukumu ya hilo? Ni ipi hukumu ya kukhitimisha Qur-aan kwa ajili yao[1]?
Jibu: Bora ni kuacha kufanya hivo kwa kutokuwepo dalili ya hilo. Lakini imewekwa katika Shari´ah kuwatolea swadaqah wale uwapendao katika jamaa zako na wengineo wakiwa ni waislamu, kuwaombea du´aa, kuwahijia na kuwafanyia ´Umrah.
Ama kuswali, kuwafanyia Twawaaf na kufanyia kisomo bora ni kuacha kufanya hivo. Hakuna dalili ya hayo. Wako wanazuoni waliojuzisha mambo hayo kwa kulinganisha na swadaqah na du´aa. Salama zaidi ni kuacha kufanya hivo. Msing katika ´ibaadah ni kukomeka na kutotumia kipimo.
[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/258-259).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 74
- Imechapishwa: 08/01/2022