8- Alimsikia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mtu akisema katika Tashahhud yake:

اللهم!إني أسألك يا الله الأحد الصَّمَدُ الذي لَمْ يَلِدْ وَلَمْ يُولَدْ وَلَمْ يَكُن لَّهُ كُفُوًا أَحَدٌ أنْ تَغْفِرَ لي ذُنوبي. إنَّكَ أنتَ الغَفورُ الرحِيمُ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba Wewe, ee Allaah, Uliye Mmoja pekee, wa milele, Usiyewahitajia waja, Ambaye hukuzaa wala hukuzaaliwa na wala hakuna yeyote unayefanana na kulingana naye, unisamehe madhambi yangu. Kwani hakika Wewe ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.”

akasema:

“Amesamehewa. Amesamehewa.”[1]

[1] Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ahmad na Ibn Khuzaymah. al-Haakim ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 161-162
  • Imechapishwa: 14/01/2019