105. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi na nne wa an-Nisaa´

al-Qummiy amesema:

“Maneno Yake:

الَّذِينَ يَتَّخِذُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۚ أَيَبْتَغُونَ عِندَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّـهِ جَمِيعًا

“Wale wanaowafanya makafiri kuwa ni marafiki wandani badala ya waumini. Je, wanatafuta utukufu kutoka kwao? [Hapana,] hakika utukufu wote uko kwa Allaah pekee.”[1]

“Bi maana nguvu. Abu ´Abdillaah amesema: “Aayah hii imeteremka juu ya Banuu Umayyah ambao walienda kinyume na Mtume wao na kutotaka kurudisha uongozi kwa Banuu Haashim.”[2]

Allaah amemtakasa Abu ´Abdillaah kutokamana na kumzulia uongo Allaah. Baatwiniyyah wanataka kuifanya Qur-aan ionekana kuwa ni yenye kuwapiga vita Banuu Umayyah, ambao hata walikuwa hawajazaliwa, kwa ajili ya Banuu Haashim, ambao hata na wao pia hawakuwepo katika wakati huo.

Aayah hii inawafedhehesha wanafiki mababu wa Baatwiniyyah ambao walikuwa wakitoa nguvu zao kutoka kwa makafiri kama wafanyavo Baatwiniyyah na Raafidhwah wanaotoa nguvu zao kutoka kwa mayahudi, manaswara, watarta na wengineo dhidi ya waislamu.

[1] 04:139

[2] Tafsiyr al-Qummiy (1/156)).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 152
  • Imechapishwa: 12/01/2018