104. Miili si chochote isipokuwa tu ni kifaa cha nyama

Mtu anatakiwa atambue kuwa kuoza kunahusiana na mwili huu wenye kuonekana na uliyofungamana. Mwili huu si chochote. Ni kifaa tu. Kinachotakiwa kutiliwa umuhimu ni yale yenye kuidhuru na kuinufaisha roho. Ibn-ul-Jawziy amepokea kwa mlolongo wa wapokezi wake:

“Baada ya Ibn-uz-Zubayr kuuawa ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) aliingia msikitini akimtafuta Asmaa´, mama yake na Ibn-uz-Zubayr, na kumwambia: “Subiri! Hivi viwiliwili si chochote. Roho ziko kwa Allaah (Ta´ala).”

Kisha Ibn-ul-Jawziy akasema:

“Tumepokea namna Ibn-uz-Zubayr alivyomwambia mama yake kabla ya kuuawa: “Mamangu! Nikifa basi ujue kuwa mimi ni nyama tu. Hayanidhuru yale yanayonipitikia.”

Khaalid bin Ma´daan amesema:

“Pindi Hishaam bin al-´Aasw alipouawa siku ya Ajnaadayn mwili wake ulianguka juu ya mwanya wa mlima na ukafungika tena. Hapakuwepo njia nyingine. Pindi waislamu walipoufikia wakakataa kuwapitisha farasi wao juu yake. Ndipo ´Amr bin al-´Aasw: “Enyi watu! Allaah amemfanya kuwa shahidi na ameipandisha roho yake. Hiki si chochote isipokuwa ni kiwiliwili tu. Waacheni farasi wapite juu yake.” Ndipo yeye mwenyewe akapita juu yake na watu wakamfuata mpaka ukawa vipande pande.”

Haya yakithibiti, basi mtu anatakiwa kutambua kwamba pindi Allaah anapouharibu mwili huu wa udongo unaopatwa na maradhi na matatizo basi kadhalika ataurudisha usipatwe na maradhi, kuupa uhai usioisha, kuupa thawabu nzuri badala ya matatizo na kuupa ujira wa milele kwa matendo yenye kukatika.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 224
  • Imechapishwa: 16/12/2016