104. Kuwatolea swaqadaqah ya chakula wazazi na jamaa

Swali 104: Tunasikia sana kuhusu chakula cha jioni cha wazazi wawili au mmoja wao na zipo njia nyingi. Baadhi ya watu wanapika chakula cha jioni khaswa katika Ramadhaan na wanawaalika baadhi ya wafanyakazi na mafukara. Wengine wanakitoa kuwapa wale wanaofutari misikitini. Wengine wanachinja kichinjwa na kuwagawia baadhi ya mafukara na baadhi ya majirani. Ni ipi sifa inayopasa ikiwa chakula hichi kinafaa[1]?

Jibu: Kuwatolea swadaqah wazazi wawili au jamaa wengine ni jambo linalofaa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema baada ya kuulizwa na muulizaji kama kuna chochote kilichobaki ambacho anaweza kuwatendea wema wazazi wake baada ya kufa kwao ambapo akajibu:

“Ndio; kuwaombea du´aa, kuwaombea msamaha, kuwatimizia ahadi zao baada yao, kuwakirimu mafariki zao na kuwaunga jamaa zao ambao hawaungiki isipokuwa kwao.”

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika miongoni mwa wema mkubwa kabisa ni mtu kuwaunga jamaa zake baba.”

Amesema pia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipomuuliza muulizaji hali ya kusema:

“Hakika mama yangu amefariki na hakuacha wasia. Je, anapata ujira nikimtolea swadaqah?” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ndio.”[2]

Vilevile kutokana na kuenea kwa maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Anapofariki mwanadamu basi matendo yake yote yanakatika isipokuwa mambo matatu; swadaqah yenye kuendelea, elimu ambayo watu wananufaika kwayo au mtoto mwema mwenye kumuombea du´aa.”[3]

Hakuna neno kuita swadaqah hii kuwa ni chakula cha jioni cha wazazi wawili au swadaqah ya wazazi wawili. Ni mamoja ni katika Ramadhaan au mwezi mwingine.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/253-154).

[2] al-Bukhaariy (1388) na Muslim (1004).

[3] Ahmad (8627) na Muslim (1631).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 73-74
  • Imechapishwa: 15/01/2022