7- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kumwambia mtu mmoja:

“Unasema nini katika swalah?” Akasema: “Husoma Tashahhud halafu nasema:

اللَّهُمَّ إِني أَسْأَلُك الْجَنَّة وَأَعُوذُ بِكَ مِنَ النَّارِ

“Ee Allaah! Hakika mimi nakuomba Pepo na najilinda Kwako kutokamana na Moto.”

Ninaapa kwa jina la Allaah kwamba siwezi kusema kile ambacho wewe na Mu´aadh mnachonong´oneza[1].” Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Tunanong´oneza hicho hicho.”[2]

[1] Bi maana du´aa yako ya ukimyakimya au maneno yako ya ukimyakimya.

[2] Abu Daawuud, Ibn Maajah na Ibn Khuzaymah (1/87/1) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swifatu Swalaat-in-Nabiy, uk. 161
  • Imechapishwa: 10/01/2019