103. Je, inafaa kuyaangaza makaburi na barabara zilizoko kati ya makaburi?

Swali 103: Je, inafaa kuyaangaza makaburi na barabara zilizoko kati ya makaburi[1]?

Jibu: Ikiwa ni kwa manufaa ya watu wakati wa kuzika au yakawa katika ukuta ni sawa. Ama kuweka mataa juu ya makaburi haijuzu. Kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale wenye kuyafanya ni mahali pa kuswalia na kuyaweka mataa.”

Ni sawa pia ikiwa mataa yamewekwa katika barabara ambayo watu wanapita karibu nayo. Ni sawa pia ikiwa kutawekwa mataa wakati inahitajika kuwaangazia wakati wanazika au wakaleta maa kwa ajili ya lengo hili.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/244-145).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 72
  • Imechapishwa: 08/01/2022