La sita: Inatakiwa kuwaheshimu wanachuoni kwa sababu wao ndio warithi wa Mitume (´alayhimus-Swalaah was-Salaam). Allaah (Ta´ala) amelinyanyua jambo lao na manzilah yao. Amesema (Ta´ala):

يَرْفَعِ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَالَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ دَرَجَاتٍ

”Allaah anawapandisha daraja wale walioamini miongoni mwenu na wale waliopewa elimu daraja za juu.” (al-Mujaadalah 58:11)

Watu hawa walimtumbukia katika jinai hii kubwa pindi alipozungumz mtu yule mwovu kwa kusema:

“Hatujapatapo kuona mfano wa wasomi wetu hawa.”

Wasomi waliokuwa wakimaanisha ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake watukufu. Makusudio ya ´wasomaji` wakati huo ni wanachuoni kwa sababu kipindi hicho yule ambaye alikuwa anasoma Qur-aan anakuwa mwanachuoni. Ama katika zama za baadaye msomaji Qur-aan anaweza kuwa hafahamu kitu katika maana ya Qur-aan. Yeye anachojua ni kusoma vizuri peke yake. Kwa sababu katika zama za mwisho wasomi watakuwa wengi na wanachuoni watakuwa wachache. Lakini katika zama za mwanzo wasomi walikuwa ni wale wanachuoni. Kwa hivyo maneno yake:

“Hatujapatapo kuona mfano wa wasomi wetu hawa.”

Bi maana wanachuoni ambao ni Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake watukufu (Radhiya Allaahu ´anhum).

Hapa tunapata faida nyingine ambayo yule anayewatukana wanachuoni- zama zozote zile – kwa sababu ya elimu yao basi anaingia ndani ya Aayah hii tukufu. Kwa sababu yule mtu alisema kwamba hatujapatapo kuona mfano wa wasomi wetu hawa. Wasomi ndio hao wanachuoni. Hili linahusu wanachuoni katika kila zama. Wanachuoni wana heshima yao na wanatakiwa kutukuzwa. Kwa kuwa wao ndio wanabeba Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanabeba elimu na wanawafikishia nayo watu. Kwa hiyo ni wajibu kuwaheshimu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ubora wa mwanachuoni ukilinganisha na mfanya ´ibaadah ni kama mfano wa mwezi ukilinganisha na nyota zengine.”[1]

“Mwanachuoni anaombewa msamaha na kila kitu mpaka samaki baharini.”

Mwanachuoni ana nafasi yake. Makusudio ya mwanachuoni ni yule anayesoma Shari´ah. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

إِنَّمَا يَخْشَى اللَّـهَ مِنْ عِبَادِهِ الْعُلَمَاءُ

”Hakika wanaomuogopa Allaah kwelikweli miongoni mwa waja wanazuoni.” (Faatwir 35:28)

Wanachuoni ndio wanamcha Allaah (Jalla wa ´Alaa) kwelikweli. Kwani wao ndio wanamjua Allaah ipasavyo. Hivyo wanamtukuza, wanamwadhimisha, kumuheshimu, kumcha na kumuogopa. Kila ambavyo elimu ya mtu inazidi ndivyo kumuogopa kwake Allaah (´Azza wa Jall) kunazidi. Kwa hiyo ni wajibu kuwaheshimu wanachuoni na kuwatukuza. Yule mwenye kuwatukana na kuwapunguza wanachuoni basi anaingia ndani ya maana ya Aayah hii:

أَبِاللَّـهِ وَآيَاتِهِ وَرَسُولِهِ كُنتُمْ تَسْتَهْزِئُونَ لَا تَعْتَذِرُوا قَدْ كَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ

“Sema:  Je, mlikuwa mnamfanyia istihizai Allaah na Aayah Zake na Mtume Wake?” Hivyo msitoe udhuru, kwani mmekwishakufuru baada ya kuamini kwenu.” (at-Tawbah 09:65-66)

[1] al-Bukhaariy (05/196), Abu Daawuud (3641), at-Tirmidhiy (2682), Ibn Maajah (223) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 132-133
  • Imechapishwa: 24/12/2018