101. Mtume alizikwa nyumbani kwake, na si msikitini kwake


Swali 101: Ni yepi maoni yako juu ya wenye kujuzisha kuswali ndani ya msikiti wenye makaburi na wakajengea hoja ya kwamba msikiti wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani yake lipo kaburi lake mteule (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)[1]?

Jibu: Abainishiwe kwamba kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) liko katika nyumba yake na si msikitini. Aliyekosea ni yule ambaye aliliingiza kaburi ndani ya msikiti.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/242).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 71
  • Imechapishwa: 08/01/2022