100. al-Qummiy upotoshaji wake wa kumi wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema:

“Muhammad bin al-Fudhwayl amepokea kutoka kwa Abul-Hasan aliyesema kuhusiana na maneno Yake:

وَلَوْلَا فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَتُهُ لَاتَّبَعْتُمُ الشَّيْطَانَ إِلَّا قَلِيلًا

“Lau si fadhila za Allaah juu yenu na rehema Zake basi hakika mngelimfuata shaytwaan isipokuwa wachache tu.”[1]

“Fadhila ni Mtume wa Alllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na rehema Zake ni kiongozi wa waumini.”

Muhammad bin al-Fudhwayl amepokea kutoka kwa mja mwema ambaye amesema:

“Rehema ni Mtume wa Allaah na fadhila ni ´Aliy bin Abiy Twaalib.”[2]

al-Qummiy amesema:

“Fadhila ni Mtume wa Alllaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na rehema Zake ni kiongozi wa waumini.”[3]

Jambo lote ni lenye kugawanywa kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kiongozi wa waumini. Huenda fungu la ´Aliy likawa kubwa na lenye uzito zaidi. Ni maoni gani Raafidhwah wanachagua? Mara fadhila za Allaah ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na rehema ni Allaah na wakati mwingine kinyume chake. Tunamuomba Allaah atukinge dhidi ya kumsemea Allaah uongo na kukipotosha Kitabu Chake kitukufu.

Fadhila na rehema za Allaah ni kule Allaah kumtuma Mtume, kuteremsha Kitabu kilicho na I´tiqaad kuu, tabia za hali ya juu na matendo mema pamoja na Allaah kuwawafikisha waumini kutoka katika Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na wale waliowafuata kwa wema kusimamia I´tiqaad, tabia na matendo haya.

[1] 04:83

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/261).

[3] Tafsiyr al-Qummiy (1/145).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 147
  • Imechapishwa: 10/01/2018