10. Yangethibiti basi tungenakiliwa


Ilipokuwa imewekwa katika Shari´ah kusimama na kujitahidi usiku wenye cheo na nyusiku za Ramadhaan ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akazindua jambo hilo na akahimiza Ummah kusimama na yeye mweneywe akafanya hivo. al-Bukhaariy na Muslim wamepokea kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Yeyote atakayesimama usiku wenye cheo kwa imani na kwa matarajio, basi Allaah atamsamehe madhambi yake yaliyotangulia.”

Endapo usiku wa nusu ya Sha´baan, usiku wa ijumaa ya kwanza ya Rajab, usiku wa Israa´ na Mi´raaj imesuniwa kuufanya maalum kwa sherehe au chochote katika ´ibaadah basi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angewaelekeza Ummah katika jambo hilo au yeye mwenyewe angefanya hivo. Iwapo angefanya chochote katika hayo basi Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wangewanukulia Ummah na wasingewaficha. Kwani wao ndio watu bora na wenye kuwatakia mema zaidi watu baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) na Allaah awawie radhi Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nao wamemridhia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 19/01/2022