10. Waislamu kuchunga wasije kutumbukia katika moja ya misingi hii


Hii ndio misingi ya kuritadi:

1- Neno la kufuru na shirki pasi na kulazimishwa.

2- Kuitakidi kufuru na  shirki.

3- Kitendo cha kufuru au shirki.

4- Kuwa na mashaka juu ya dini na yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Mambo haya ni lazima kwa waislamu wote na khaswa wanafunzi wayatilie umuhimu kutokana na wingi wa fitina, maovu, shubuha, siku hizi. Vilevile walinganizi waovu na upotevu wamekuw wengi hii leo. Kwa hivyo ni lazima kwa muislamu aliwekee umuhimu jambo hili ili asitoke katika dini yake kwa kufanya kitu katika hayo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 24
  • Imechapishwa: 06/05/2018