Miongoni mwa haki za wanandoa wakati wa uchumba ni ukweli na waelezane juu ya sifa zao ambazo ni muhimu katika ndoa. Mtume wetu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muuzaji na mnunuwaji wana uwezo wa kubadili maadamu hawajatengana. Ikiwa ni wakweli na wacha-Mungu basi watabarikiwa katika biashara yao. Na lau watadanganya na kuficha baraka itaondoshwa kwenye biashara yao.”[1]

Ikiwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema hivi juu ya mabadilisho ya biashara, unafikiriaje inapohusiana na ndoa ambayo ina mu´amala wenye kudumu? Ni jambo lisokuwa na shaka ya kwamba mtu anapaswa awe mkweli na mcha-Mungu. Sawa ikiwa ni mwanamke au mwanaume anaficha kitu muhimu ni usaliti kwa yule mwingine. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mwenye kutufanyia ghushi sio katika sisi.”[2]

[1] al-Bukhaariy (2079) na Muslim (1532

[2] at-Tirmidhiy (1315) na Muslim (102) kwa muundo: “Mwenye kufanya ghushi sio katika sisi.”

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 24/03/2017