10. Sharti ya saba ya swalah


Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya saba ni kuingia kwa wakati. Dalili ya hilo ni kutoka katika Sunnah kwenye Hadiyth ya Jibriyl (´alayhis-Salaam) alipomswalisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanzoni mwa wakati wa swalah na mwishoni wa wakati wake. Akasema:

“Ewe Muhammad! Swalah ni baina ya nyakati hizi mbili.”[1]

Kadhalika Amesema (Ta´ala):

إِنَّ الصَّلاَةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا

“Hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekewa nyakati maalumu.”

Bi maana imefaradhishwa kwa wakati wake. Dalili ya kuingia kwa wakati wake ni Kauli Yake (Ta´ala):

أَقِمِ الصَّلاَةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَى غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا

“Simamisha swalah pale jua linapoanza kupinduka mpaka kiza cha usiku na swalah ya alfajiri; hakika swalah ya alfajiri ni yenye kushuhudiwa.”

MAELEZO

Ni lazima swalah iswaliwe ndani ya wakati. Kwa sababu Allaah amefaradhisha swalah kwa nyakati zake. Swalah haitosihi iwapo itaswaliwa kabla ya kuingia wakati wake. Akiiswali baada ya kutoka wakati wake kwa kukusudia anapata dhambi. Isipokuwa ikiwa kama inafaa kwake kuichelewesha kwa sababu ya udhuru kama safari au maradhi. Katika hali hiyo ataichelewesha Dhuhr pamoja na ´Aswr na Maghrib pamoja na ´Ishaa. Hapo hakuna neno. Vinginevyo haijuzu kufanya hivo pasi na udhuru au kuswali kabla ya wakati. Swalah haisihi akiswali kabla ya kuingia wakati. Isipokuwa ikiwa kama ataikusanya na swalah nyingine ya baada yake kwa sababu ya safari au maradhi. Katika hali hiyo hakuna neno.

[1] Abu Daawuud (393) na tamko ni lake, at-Tirmidhiy (149), Ahmad (3081), Ibn Khuzaymah (325), al-Haakim (17193) na wengineo. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud (377).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 82
  • Imechapishwa: 30/06/2018