10. Ni ipi hukumu ya matendo ya waja?

Swali 10: Ni ipi hukumu ya matendo ya waja?

Jibu: Matendo ya waja yote, ya utiifu na maasi, yanaingia katika uumbaji wa Allaah, mipango na makadirio.

Hata hivyo wao ndio wenye kuyafanya. Allaah hakuwalazimisha nayo. Wanayafanya kwa kutaka kwao na kwa uwezo wao.

Ni matendo yao kihakika. Wanasifiwa na kulipwa kwayo na kuadhibiwa kwayo.

Matendo ni uumbaji wa Allaah kihakika. Allaah amewaumba, akaumba matakwa yao, uwezo wao na yote yanayopitika kwa hilo.

Tunaamini maandiko yote ya Qur-aan na Sunnah yenye kuthibitisha ueneaji wa uumbaji na uwezo wa Allaah juu ya kila kilichopo na kupitika.

Hali kadhalika tunaamini maandiko yote ya Qur-aan na Sunnah yenye kuthibitisha kuwa ni waja ndio wenye kufanya matendo mazuri na mabaya na kwamba wao wenyewe ndio wenye kuchagua matendo yao. Allaah ameumba nguvu na matakwa yao. Mambo hayo mawili ndio sababu ya kupatikana matendo yao na maneno yao. Yule mwenye kuumba sababu anaumba pia chenye kusababishwa. Allaah ni mkubwa na mwadilifu kuwatenza nguvu matendo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Naaswir as-Sa´diy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahamm-ul-Muhimmaat, uk. 56
  • Imechapishwa: 25/03/2017