Swali 10: Ni ipi hukumu ya hafla za kuaga zinazokuwa na mchanganyiko kati ya jinsia mbili? Ni ipi hukumu ya kujitibu kwa muziki?

Jibu: Hafla haziwi mchanganyiko. Bali ni lazima kuwepo hafla za wanaume kwa wanaume peke yao na za wanawake kwa wanawake peke yao. Kuhusu mchanganyiko ni maovu na ni miongoni mwa matendo ya watu wa kipindi cha kikafiri.

Ama kujitibu kwa muziki ni jambo halina msingi wowote. Bali ni miongoni mwa matendo ya wapumbavu. Muziki sio dawa bali ni ugonjwa. Ni katika ala za pumbao. Muziki aina zote ni maradhi kwa moyo na ni sababu ya kupondoka kwa tabia. Dawa yenye kufaa na yenye kumfanya mgonjwa akastareheka moyo wake ni yeye kusikiliza Qur-aan, mawaidha yenye faida na Hadiyth zenye manufaa. Ama kujitibu kwa muziki na nyenzo zengine za pumbao ni miongoni mwa mambo yanayowapelekea katika upotofu na kuwazidishia maradhi juu ya mengine na kadhalika kunawafanya wanahisi uzito kusikiliza Qur-aan na mawaidha yenye faida.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Mariydhw, uk. 31
  • Imechapishwa: 19/05/2019