3- Hedhi na damu ya uzazi. Mwanamke ambaye inamtoka hedhi yake au damu yake ya uzazi basi anatakiwa kula katika Ramadhaan kwa njia ya ulazima. Ni haramu kwake kufunga. Akifunga haitosihi kutoka kwake. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliyesema:

“Je, anapopata hedhi si haswali wala hafungi? Huo ni katika upungufu wa dini yake.”[1]

Ni lazima kwake baadaye kulipa. Hilo ni kutokana na maneno ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:

“Hilo lilikuwa linatupata ambapo tunaamrishwa kulipa swawm na hatuamrishwi kulipa swalah.”[2]

[1] al-Bukhaariy (304).

[2] Muslim (335).

  • Mhusika: Nukhbatin minal-´Ulamaa´
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fiqh-ul-Muyassar, uk. 155-156
  • Imechapishwa: 23/04/2020