10. Murji-ah wanavutia katika madhambi na wanachukulia usahali matendo

Murji-ah waliopindukia na Murji-ah al-Fuqahaa´ wote wawili wanavutia katika maasi na kuchukulia usahali matendo. Wanavutia Qur-aan na Sunnah kukhalifiwa. Pindi Aayah zinapotaja kupanda kwa imani wanazikengeusha kwa matamanio yao na kwa hivyo wanatumbukia katika madhambi makubwa. Vivyo hviyo wanafanya na Hadiyth kuhusu uombezi. Hili tu linatosheleza kuonyesha namna ya ubaya wa madhehebu ya Murji-ah al-Fuqahaa´.

Pamoja na hivyo kuna tofauti kati ya wao na wale wenye kusema kuwa imani ni utambuzi peke yake. Katika tafsiri yao kunaingia shaytwaan, Fir´awn, Nimrud na wengine katika majangiri makafiri wakubwa walio na ukafiri aina mbaya kabisa. Watu wote wanamtambua Allaah (´Azza wa Jall). Abu Jahl alikuwa anamtambua Allaah ni nani na akikubali kuwa Yeye ndiye Muumbaji wa mbingu na ardhi. Pamoja na hivyo walikuwa ni katika makafiri wabaya kabisa.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qurrat-ul-´Aynayn bi Tawdhwiyh Ma´aaniy ´Aqiydat-ir-Raaziyayn, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 15/10/2016