[18] Inatakiwa kuamini vilevile kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Mtume wetu, Nabii wa mwisho, bwana wa Mitume, kiongozi wa wachaji na mjumbe wa Mola wa walimwengu.

Amemtumiliza kwetu na kwa viumbe wengine wote. Yeye ndiye bwana wa wana wa Aadam na ndiye wa kwanza atakayefufuliwa na ardhi. Aadam na walioko chini yake watakuwa chini ya bendera yake. Yeye ndiye shahidi wa kila Mtume na ndiye shahidi wa kila Ummah. Allaah (Ta´ala) amechukua mkataba kwa Mitume kumwamini, kutoa bishara njema juu yake, kumwelezea na kumbainisha katika vitabu vyao pamoja na zile alama na miujiza yenye kugonga ambayo Allaah alimtunuku kabla na baada ya kupewa utume.

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 35
  • Imechapishwa: 25/02/2019