10. Mtu aliye nyuma ya vurugu iliyoko hii leo


Mtu wa kwanza kuzusha uasi kwa watawala wakati wa sasa ilikuwa ni Hasan al-Bannaa. Alifanya hivo kwa njia ya maandamano na mapinduzi. Nilikuwa bado kijana mdogo pindi Hasan al-Bannaa alipojitokeza uwanjani. Akaunda al-Ikhwaan al-Muslimuun. Nilikuwa na umri wa miaka tisa wakati nilipokuwa nikienda na genge la al-Ikhwaan kwenye ikulu ya mfalme wa Misri Fu´aad wa wakati huo na kusema:

“Rudi Ankara!”

Kwa sababu alikuwa na asli ya kutoka Uturuku.

1936 nikajiunga na Answaar-us-Sunnah. Baadhi ya marafiki zangu wa karibu ilikuwa ni vijana watatu wakiitwa Hasan Jamaaliy, Muhammad Munjiy na Muhammad Bashshaar. Hawa watatu walikuwa ni katika shirika la siri la al-Ikhwaan al-Muslimuun pamoja na kuwa walikuwa na ´Aqiydah ya Salaf. Hasan Jamaaliy na Muhammad Munjiy walikuwa siku zote wakionyesha wazi wazi ´Aqiydah ya Salafiyyah. Hasan al-Bannaa akiwapaka mafuta kwa kuwatajia Ibn Taymiyyah, Ibn-u-Qayyim na Ibn ´Abdil-Wahhaab. Hili ni katika ajabu yao. Walikuwa wakitambua Salafiyyah pasina kuitendea kazi. Ni kama baadhi ya watu leo wanaosema kuwa ni Salafiyyuun.

Wakakodi nyumba kwenye mashamba ya mitende ili kutengeneza mabomu. Hasan Jamaaliy ndiye alikuwa shujaa zaidi. Yeye ndiye alikuwa akivaa mabomu na kuyarusha kwenye maduka na katika jamii. Haya ndio yalikuwa matendo ya Hasan al-Bannaa. Alikuwa anajua Tawhiyd na shirki, lakini katu hazungumzi juu yake. Nilikuwa na rafiki anayeitwa Sayyid Sa´d kutoka Ismaa´iyliyyah. Hasan al-Bannaa alikuwa akitangamana na watu wenye kuomba uokovu mwingine asiyekuwa Allaah, akidai kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameumbwa kwa nuru na wakiamini mambo ya hirizi. Sayyid Sa´d alimwambia: “Je, hii si shirki?” Siuwakataze kufanya hivo?” Hasan al-Bannaa alikuwa akijibu: “Baadae. Huu sio wakati wake sasa.” Kisha anamwambia: “Vipi itakuwa msimamo wako mbele ya Allaah lau utakufa kabla hujawafunza?” Hasan al-Bannaa anajibu: “Najua nitakavyojibu.” Hapo ndipo Sayyid Sa´d husimama na kumwacha al-Bannaa[1].

[1] at-Tafjiyraat, ya Abu ´Abdil-A´laa,uk. 5:6.

Mwandishi: Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Bannaa
Marejeo: Lamahaat ´an Da´wat-il-Ikhwaan al-Muslimiyn, uk. 32-33
Mkusanyaji: Muhammad bin ´Iwadhw bin ´Abdil-Ghaniy