Katika kumuamini Allaah kunaingia vilevile kuitakidi kuwa imani ni maneno na matendo. Imani inazidi kwa utiifu na inapungua kwa maasi na kwamba haijuzu kumkufurisha muislamu yeyote kwa dhambi aliyoifanya ilio chini ya shirki na kufuru. Mfano wa dhambi hizo ni kama uzinzi, kuiba, kula ribaa, kunywa pombe, kuwaasi wazazi na dhambi nyenginezo kubwa midhali hajahalalisha hayo. Amesema (Subhaanah):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.” (04:48)

Vilevile kutokana na yale yaliyothibiti katika Hadiyth zilizopokelewa kwa mapokezi mengi kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba Allaah atawatoa Motoni wale ambao moyoni mwao walikuwa na imani sawa na uzito wa mbegu ya haradali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah as-Swahiyhah wa maa yudhwaadduhaa, uk. 10
  • Imechapishwa: 30/05/2023