10. Msimamo kwa walinganizi juu ya vitabu vya Fiqh

Ni wajibu kwa wanachuoni na khaswa wale wanaoeneza kati ya watu Fiqh na fataawaa zao wasiwe na ujasiri wa kutumia dalili Hadiyth isipokuwa baada ya kuhakikisha kuthibiti kwake. Vitabu vya Fiqh wanavyorejelea kama kawaida vimejaa Hadiyth nyingi ambazo ni dhaifu, zenye kukataliwa na zengine ambazo hazina hata msingi. Hilo linatambulika kwa wanachuoni. Nilikuwa nimeanza mradi ambao kwangu naonelea kuwa ni muhimu sana kwa wale wenye kujishughulisha na Fiqh na kuupa anwani “al-Ahaadith adh-Dhwa´iyfah wal-Mawdhwu´ah fiy ummahaat al-Kutub al-Fiqhiyyah” na nikikusudia kwa anwani hiyo vitabu vifuatavyo:

1- “al-Hidaayah” cha al-Marghiynaaniy katika Fiqh ya Hanafiy.

2- “al-Mudawwanah” cha Ibn-ul-Qaasim katika Fiqh ya Maalikiy.

3- “Sharh-ul-Wajiyz” cha ar-Raafi´iy katika Fiqh ya ash-Shaafi´iy.

4- “al-Mugniy” cha Ibn Qudaamah katika Fiqh ya al-Hanbaliy.

5- “al-Bidaayah al-Mujtahid” cha Ibn Rushd al-Andalusiy.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manzilat-us-Sunnah fiyl-Islaam, uk. 19-20
  • Imechapishwa: 10/02/2017