10. Mkusanyiko katika msikiti wa hospitali au kwenda katika misikiti mikubwa nje ya hospitali?

Swali 10: Hospitali kunafanywa swalah nyingi za mkusanyiko ilihali misikiti iko karibu. Je, inalazimu kutokana na ukaribu wake kwenda msikitini au mtu atosheke na swalah za mkusanyiko hizi ndani ya hospitali[1]?

Jibu: Ni kitu kinahitaji upambanuzi. Ambaye analazimika kuwepo hospitalini, kama mfano wa mlinzi na wengineo, au mgonjwa ambaye hawezi kufika msikitini, basi haitomlazimu kutoka kwenda msikitini. Bali ataswali mahali pake pamoja na mkusanyiko ambao anaweza kuswali pamoja nao. Kuhusu ambaye anaweza kufika msikitini kutamlazimu kwake kufanya hivo kwa kutendea kazi dalili za ki-Shari´ah. Miongoni mwazo ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote atakayesikia adhaana na asiitikie basi hana swalah isipokuwa akiwa na udhuru.”[2]

Akaulizwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa): “Ni udhuru upi?” Akasema: “Khofu au maradhi.”

Ameipokea Ibn Maajah, ad-Daaraqutwniy, Ibn Hibbaan na al-Haakim kwa cheni ya wapokezi Swahiyh.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (12/67).

[2] Ibn Maajah (785).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam Swalaat-il-Jumu´ah wal-Jamaa´ah, uk. 36-37
  • Imechapishwa: 26/11/2021